Rais Uhuru awatuma mawaziri wote likizo ya mapumziko
Rais Uhuru Kenyatta amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko.
Likizo hiyo ya siku 11 itaanza Jumatatu, Agosti 17 hadi Agosti 28 kulingana na taarifa kutoka Ikulu.
Habari Nyingine: Makachero wawili wa DCI wasombwa na mafuriko Kericho

Aidha katibu wasimamizi na katibu wa kudumu pia wametakiwa kuenda nyumbani kupumzika kwa kipindi hicho.
Duru zinaarifu huenda hatua hiyo ni kumuwezesha Rais kutangaza baraza lipya la mawaziri.
Barua kutoka kwa mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua ilisema kwa kipindi hicho cha likizo kamati zote za mawaziri hazitakuwa na vikao.
Habari Nyingine: Jumamosi Agosti 15: Maambukizi ya Covid-19 yarekodi watu 515 zaidi

Hata hivyo, kinyua alisema mawaziri watatarajiwa kutekeleza majukumu ya nyadhifa zao.
Mawaziri hao, Kinyua alisema, wataruhusiwa kutokuwa afisini lakini ni lazima wapate ruhusa kutoka kwa rais iwapo mtu anataka kusafiri kuenda nje ya nchi.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIFzgZJmqZqho2LCqcHRrmSar5Gpwq6tjKaYsJmqnr%2Bqedaoq55lnJ64qsbOZrCaZZ2Wvba52aKiqGaYqbqt